Kitalu cha miti Makuyuni

Posted on 04/22/2026
|

Huku taifa likilenga kupanda miti bilioni kumi na tano ifikiapo mwaka wa 2032, wakazi wa Mukuyuni huko Makueni wamepokea mafunzo ya jinsi ya kukuza miche aina mbalimbali kwa njia nzuri ili kuhakikisha miche inapopandwa inastahimili mazingira magumu.
Mafunzo hayo yalitolewa wakati wa uzinduzi wa kitalu cha kisasa cha shirika la PALMA ambacho kina uwezo wa kuzalisha miche elfu mia mbili hamsini kwa wakati mmoja .