Kizazaa kilizuka mjini Kisii usiku wa kuamkia leo baada ya mamia ya vijana ambao wamekuwa wakipokea mafunzo kuhusu mradi wa Nyota kulazimika kulala ndani ya shule ya msingi ya Kisii kutokana na mzozo wa malipo na maafisa wanaosimamia shughuli hiyo Nyaribari Chache.
Vijana hao walizua vurugu mwendo wa saa mbili hadi saa sita usiku wa manane wakidai kuhadaiwa kwa kulipwa shilingi mia tatu badala ya elfu moja kama walioahidiwa. Ilibidi maafisa wa usalama kutoka kituo cha polisi cha Kisii kuingilia kati na kutuliza hali .