Serikali ya Kaunti ya Laikipia imetoa shilingi milioni 75 za basari na ufadhili kwa wanafunzi wenye mahitaji mbalimbali katika wadi zote 15, hatua inayowawezesha wanafunzi kutoka familia zenye kipato cha chini kuendelea na masomo bila kusitishwa.
Mpango huu utapunguza mzigo wa karo, sare na mahitaji ya shule, na kusaidia familia hizo kumudu gharama za elimu na kupunguza visa vya wanafunzi kuacha shule. Gavana wa Laikipia Joshua Irungu alieleza kuwa msaada huu utasaidia kuinua viwango vya elimu na kuwapa wanafunzi fursa sawa za kupata elimu na hatimaye ajira na kujitegemea.