Serikali yaongeza vivutio vya watalii kaunti ya Kwale

Posted on 04/22/2026
|

Wizara ya utalii na wanyapori ikishirikiana na taasisi ya utafiti na mafunzo ya wanyapori zimezindua kituo cha jamii cha utalii cha njia za mbao za kuelea kwenye msitu wa mikoko katika eneo la Chale kaunti ya Kwale.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo, waziri wa utalii Rebecca Miano amesema asilimia 50 ya watalii wanaozuru Pwani hutembelea kaunti ya Kwale kutokana na wingi wa vivutio na hivyo kuna haja ya kuendelea kuwekeza katika vivutio zaidi.