Wizara ya ICT yachukua jukumu la kuhifadhi kinamasi Nandi

Posted on 04/22/2026
|

Wizara ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano imeanza mchakato wa kurejesha sehemu ya kinamasi cha King’wal kilichoko katika Kaunti ya Nandi.
Rasilmali hiyo ya asili imeharibiwa mno na shughuli za kilimo hali inayotishia uhai wa viumbe mbalimbali wanaoitegemea, wakiwemo swara adimu aina ya Sitatunga. Serikali ya Kaunti ya Nandi ilitoa sehemu ya kinamasi hicho kwa wizara ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa shughuli za uhifadhi wa mazingira.